Header Ads

TAMASHA kubwa la NYANZA Featival linatarajia kuanza kusaka vipaji mtaa kwa mtaa


Displaying IMG-20170116-WA0021.jpg



TAMASHA kubwa la NYANZA Featival linatarajia kuanza kusaka vipaji mtaa kwa mtaa lengo likiwa ni kuhakikisha wanawafikia wasanii wote chipukizi katika Nyanja zote za Music, Scratch dj, Dancer , Mitindo, Uigizaji na uchekeshaji.

Akiongea na wanahabari mwenyekiti wa kamati ya maandalizi Fabian Fanuel wa alisema lengo ni kuhakikisha wanaibua vipaji vyote na kuviendeleza.

“Ni muda sasa wasanii ambao ni underground wamekosa nafasi ya kupanda jukwaa  moja na wasanii wenye majina  makubwa ,licha ya jiji hili kuwa na wasanii wengi na waliosheheni vipaji mbalimbali katika Nyanja zote”, alisema Fanuel.

Fanuel alisema kuwa wanatarajia kuanzia mitaa ya Dampo, Igoma,  Mkuyuni , Nyegezi Buhongwa,  Mabatini,  Kisesa,  Sahara,  Buzuruga , National, Furahisa, Pasiansi Ilemela, Igombe, Kiseke na Kiloleli.

“Sisi kama waandaaji tumejipanga vya kutosha kuhakikisha wasanii wa Mwanza wanatangaza vipaji vyao ni kazi itakuwa imebaki kwao tu kuhakikisha waitendea haki fursa hii ambayo ni adimu kuipata tena”, alisema Fanuel.

Alisema litakuwa tamasha la aina yake kutokana na maandalizi na kuwataka wafadhili kuendeza kujitokza katika kuhakikisha wanafanikisha tukio hilo muhimu linalotajia kufanyika katika sherehe za sikukuu za Pasaka kwenye uwanja wa CCM Kirumba.


Nyanza Festival 2017 linatorajariwa kufanyika kwa mara ya kwanza Jijini Mwanza na baadaye kusambaa katika mikoa ya Kanda ya Ziwa, Tanzania na nje ya Tanzania ikiwashirikisha wasanii wote kutoka jijini hapa.

Hivi karibuni Bodi ya filamu nchini ,kupitia katibu wake  Joyce Fisoo ilitua jijini hapa kutoa mafunzo kwa wadau na wasanii chipukizi  lengo la kuwajengea uwezo katika stadi za uzalishaji, uuzaji na usambazaji  wa kazi zao.

imeandikwa na mwandishi wetu wa KALIZOTE BLOG Na James Timber KUTOKA Mwanza

No comments