Header Ads

Watu watano waambukizwa Ukimwi hospitalini ya China

Image result for picha ya ukimwi

Hospitali moja nchini Uchina imekiri kwamba watu watano waliambukizwa virusi vinavyosababisha Ukimwi hospitalini humo kimakosa.
Waliambukizwa na mhudumu wa afya ambaye alitumia tena vifaa vya matibabu ambavyo vilifaa kutupwa baada ya kutumiwa.
Maafisa wanasema mhudumu huyo alitumia bomba lililotumiwa kumtibu mgonjwa mwenye Ukimwi kwa wagonjwa wengine.
Maafisa wa utawala wa mkoa wametaja kisa hicho kama "ukiukaji mkubwa wa utaratibu".
Tayari wahudumu watano wamefutwa kazi katika hospitali hiyo ya mkoa ya Zhejiang katika mkoa wa Hangzhou.
Maafisa hao wa afya wa mkoa wamesema walifahamishwa kuhusu kisa hicho 26 Januari.
Lakini kwenye taarifa, hawajasema iwapo kuna wagonjwa wengine ambao huenda waliwekwa kwenye hatari ya kuambukizwa na ni maradhi ya aina gani wale walioambukizwa walikuwa wakitibiwa.
Wale walioambukizwa watapokea matibabu na fidia, taarifa fupi ilisema.
Katika ripoti ya hivi karibuni, China ilisema kulikuwa na watu 501,000 waliokuwa wameambukizwa virusi vya Ukimwi kufikia mwaka 2014




chanzo bbc

No comments