Header Ads

Jinsi ya kuondokana na hisia pamoja na mvunjiko wa moyo mara baada ya kuachwa au kuachana kwenye mahusiano ya kimapenzi.



Image result for jinsi ya kuzuia kuachana


Hisia huchanganywa zaidi na vitu mlivyokua navyo na kutumia wote kwa pamoja kama mapenzi, sehemu mlizokua mmezoea kwenda wote na hata sehemu mliokua mkilala pamoja, labda kitu kinachoumiza kichwa zaidi hata kama ilikua lazima uhusiano kuvunjika iwe kwa kumfumania au la, ni ugumu wa kuondoka kwa hisia ulizonazo pamoja na kumbukumbu za maisha yenu mlivyokua wapenzi na kuendelea na maisha ya kawaida.
kiumeni.com tumekutafutia na kuweka pamoja njia ya kukurudisha na kuondokana na mvunjiko wa moyo na hisia katika kipindi hiki kigumu cha kuachwa na kukurudisha katika hali ya kawaida ya maisha...
  • Mtoe kwenye hio nafasi uliokua umemweka...
Kitu cha kwanza acha kuhisi kuwa mpenzi wako huyo alikua ni zawadi toka kwa Mungu, maana najua unajua kabisa alikua hajakamilika, na kama tukiwa wa kweli hakuwa anafikia hata karibu ya kitu kizuri na mapungufu yake ni mengi ndo maana mpaka sasa hivi uko kwenye hii hali, tengeneza orodha ya vitu na tabia zote ambazo ni vibaya kuhusu yeye na karibisha rafiki zako wakusaidie.
  • Hakikisha wakati mnaachana makubaliano ya pande zote mbili yamefikiwa...
Kuwa na uhakika kwamba mmesha achana na hamuwezi kurudiana tena na ndo mwisho wa mahusiano yenu na wala sio likizo inasaidia sana kukutuliza hisia na kuondokana na matumaini hewa, na kama kuna kitu chochote cha kuweka sawa ungeweka sawa sasa hivi maana ndo mwisho wa ukurasa wa uhusiano.
  • Usijaribu kumpigia simu...
Hata kama ukimpigia simu haito saidia, sana sana utakua unajiumiza moyo kwa hisia unazozisababisha, na hii ndo nguzo kubwa ya kutumia ili undokane na mpasuko wa moyo, baada ya kuwa nae kwa kipindi kirefu namba yake ndo namba ulioipiga mara nyingi zaidi, kwa hio kwa vyovyote vile hisia zitakua zinakutuma kwa hali ya juu ili ufanye hivi, cha kufanya hakikisha umeifuta namba yake, na kama ukimpigia simu utajikuta unajiongezea miezi ya kutomsahau na kuumia kwa msongo wa mawazo, na mtoe kwenye orodha ya marafiki zako wa facebook, fikiri ukiwa facebook  ukaona picha yake akiwa amekumbatiwa na mwanaume mwingine, nadhani unakiona kwanini mwanzo mpya ni muhimu.
  • Fanya mazoezi...
Bila mpenzi wako kukushika mkia, sasa hivi una muda wa kutosha kufanya mazoezi na kujiweka mweili katika hali nzuri, mazoezi ni mazuri kwa afya yako na ni njia nzuri ya kuondokana na hisia, ukiwa na mwili mzuri ni kitu kizuri cha kuvutia wasichana wapya.
  • Kaa mbali na marafiki zake pamoja na sehemu anazopendelea...
Kama unataka kuondokana na hisia zitokanazo na kukutana na mpenzi wako wa zamani kwa mda huu, inabidi ujitoe kwa baadhi ya mambo, inabidi ukate mawasiliano na baadhi ya marafiki ambao wapo upande wake na kuachana kabisa na baadhi ya sehemu mlizokua mnapendelea kwenda. Ni vitu vidogo kuvitoa kama utakuwa unahitaji pumziko la hisia, mawazo na akili yako kwa ujumla.
  • Tupa mbali kumbukumbu zozote zinazokukumbusha wewe na yeye...
Hilo doli, kadi na hayo maua aliyokupa kwa ajili ya siku yako ya kuzaliwa, hilo shati alilokununulia, hizo picha zilizotoka vizuri za yeye na wewe, ondoa zote na eiza uzitupe au uweke mbali, utavyoharakisha kutoa hivyo vitu ndo utakavyo sahau kwa haraka zaidi na kabla hujauliza "ndio", unaweza acha vitu ambavyo havikuletei hisia yeyote, ila nguo zake, vito vya kuvaa na vingine vyovyote vinavyo kukumbusha mbali viondoe.
  • Usijaribu kufata vitu vyako...
Usijaribu kufata vitu vyako, nguo, cd na kila kitu kingine, jaribu kuviwazia kama umevipoteza, iwapo ukiviendea utajisababishia mjazo wa hisia usioutaka, jaribu kukaa mbali nae kwanza kwa sasa, ni bei rahisi kulipia kuliko kwenda na kumkuta anamawazo au hasira na kusababisha vitu vingine ambavyo ungeviepuka kama usinge kwenda. 
  • Tumia muda na marafiki zako...
Mapenzi hutusahaulisha marafiki, tunakosa mda kabisa wa kutumia pamoja na marafiki maana wapenzi wetu hututaka tutumie muda zaidi na wao, lakini sasa hivi upo singo ni vizuri ukatumia muda wako na washikaji, na kufanya mambo yanayo kuburudisha, ukitumia muda upo bize na mambo ya kukufurahisha huwezi pata muda wa kumuwaza tena.
  • Kumbuka mambo mabaya kuhusu yeye...
Hisia hazikimbiwi, hata zikipita siku baada ya kuachana, unaweza kujikuta unaanza kumuwaza, cha kufanya ukijikuta hivyo anza kufikiria mabaya yote kuhusu yeye, nyakati alizokua anakuboa, jinsi mlivyokua mnagombana, tabia zake ulizokua huzipendi, hii itakusaidia kuondokana na hisia za kumkumbuka.
  • Tumia vyema uhuru wako ulionao sasa na jiachie...
Mahusiano huwa ni kijitoa na kujifunga ili kumfurahisha mpenzio, kuwa singo kunatakiwa kuwe juu ya kujirusha na kujiachia na kufanya kitu chochote ambacho unajisikia kufanya, kama ni kwenda klabu, nenda. Fanya yote na rudisha furaha yako na msahau kwa yote mabaya alionayo.
  • Fanya mapenzi na msichana mwingine...
Moja kati ya njia zilizo na uhakika zaidi kufanya kazi ni kufanya mapenzi na msichana mwingine, maana sababu kubwa inayotufanya kutoachana na hisia za mpenzi wa zamani ni hofu jinsi ya kumpata msichana mpya, ndo kitu kikubwa kinachoturudisha nyuma kwenye mazingira tuliyoyazoea. Kumtafuta msichana mpya au upendo mpya hata kama ni wa siku moja ni njia nzuri ya kuondokana na mvunjiko wa hisia.

No comments