Mkuu wa wilaya ya Shinyanga JOSEPHINE MATIRO anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika kongamano la maombi la wanafunzi wa
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga JOSEPHINE MATIRO anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika kongamano la maombi la wanafunzi wa vyuo na sekondari mkoani Shinyanga linalotarajiwa kufanyika jumamosi wiki hii.
Kwa mujibu wa mwandaaji wa kongamano hilo HAPPY MWAJA ambaye pia ni mkurugenzi wa EASYFLEX PRODUCTION STUDIO,kongamano hilo litaanza majira ya saa nne asubuhi katika chuo cha ushirika Moshi tawi la Kizumbi Shinyanga na litawakutanisha wanafunzi kutoka katika vyuo na shule mbalimbali zilizopo katika mkoa wa Shinyanga.
Bi.MWAJA amesema lengo la kongamano hilo pamoja na mambo mengine,ni kuwajengea vijana hofu ya Mungu na kutengeneza umoja wa Kimunngu pamoja na kuombea maendeleo ya elimu kwa mkoa.
Viongozi wa dini kutoka madhehebu mabalimbali ya Kikristu wanatarajiwa kuhudhuria kongamano hilo.
Post a Comment