Header Ads

Hatimaye bondia wa Tanzania Mohammed Matumla ametakiwa kupumzika kwa muda wa miezi 10

Matumla
Hatimaye bondia wa Tanzania Mohammed Matumla ametakiwa kupumzika kwa muda wa miezi 10 hadi 12 kufuatia kupigwa kwa Knockout (KO) na kupata maumivu makali ya kichwa na mpinzani wake bondia Mfaume Mfaume na kupelekea kufanyiwa upasuaji katika pambano lisilo la ubingwa .
Matumla alilazimika kukimbizwa hospitali baada ya raundi 10 na ya mwisho kupigwa KO mbaya kufuatia kusukumiwa makonde mazito na mpinzani wake.
Mtoto huyo wa bondia gwiji wa zamani nchini, Rashid Matumla alifikishiwa chumba cha wagonjwa mahututi (ICU) katika hospitali ya Muhimbili, kabla ya kutolewa na kuwekwa wadi ya kawaida.
Kwa sasa mwana ndinga huyo anaendeea vizuri huku akiendelea kupatiwa matibabu katika hospaitali ya taifa ya muhimbili jijini Dar es salaam chini ya uangalizi mkubwa wa madaktari.

No comments