Mkuu wa wilaya ya Shinyanga amefanya ziara ya kushitukiza katika soko
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga amefanya ziara ya kushitukiza katika soko la nguzo nane mjini Shinyanga kwa lengo la kukagua usafi wa mazingira na miundo mbinu katika soko hilo
Akiwa katika soko hilo Mheshimiwa Matiro ameagiza uongozi wa soko kukaa na kuweka mikakati ya kuboresha vibanda wanavyofanyia biashara ili viwe vya kisasa zaidi.
Mheshimiwa Matiro amesisitiza suara la usafi wa mazingira katika soko hilo kwa ajili ya usalama wa afya za wateja wanaopata huduma mahali hapo,lakini pia wafanyabiashara wenyewe
Amesema serikali haitosita kusitisha uendeshaji wa shughuli katika soko hilo iwapo wafanya biashara hawatozingatia kanuni za afya na usafi wa mazingira.
Kwa upande wao wafanya biashara wanaofanya shughuli katika soko hilo wamekiri kuwepo uchafu wa mazingira katika maeneo wanayofanyia kazi na kuahidi kubadilika na kuzingatia kanuni za afya na usafi wa mazingira.
Mwenyekiti wa soko la Nguzo nane Hassan Baruti ameahidi kutekeleza maagizo yaliyotolewa na mkuu wa wilaya,na kuomba kila mfanyabiashara kutimiza wajibu wake,kutii sheria na kanuni zilizopo kwa mujibu wa mwongozo.
Katika ziara yake hiyo katika soko la Nguzo nane Mkuu huyo wa Wilaya ya Shinyanga amewataka maafisa afya kuwajibika katika nafasi zao,kusimamia usafi wa mazingira ili kudhibiti hali ya uchafu ambao unaweza kusababisha mlipuko wa magonjwa kama vile kipindupindu.
Post a Comment