Header Ads

Waziri MWAKYEMBE azungumzia madaraka ya wakuu wa Mikoa na Wilaya

Waziri wa Katiba na sheria Dakta HARRISON MWAKYEMBE ametoa ufafanuzi kuhusu madaraka ya wakuu wa mikoa na wilaya na kusema yapo kwa mujibu wa katiba na kutambuliwa kuwa mwakilishi wa rais katika eneo lake husika.

Waziri wa Katiba na sheria, Dakta HARRISON MWAKYEMBE
Waziri wa Katiba na sheria Dakta HARRISON MWAKYEMBE ametoa ufafanuzi kuhusu madaraka ya wakuu wa mikoa na wilaya na kusema yapo kwa mujibu wa katiba  na kutambuliwa kuwa mwakilishi wa rais katika eneo lake husika.

Akizungumza katika mahojiano na TBC Dakta MWAKYEMBE amesema Sheria ya Tawala za mikoa namba 19 ya mwaka 1997 kifungu cha TANO  na cha sita vinamtambua mkuu wa mkoa kuwa anaweza kukasimiwa madaraka yoyote na rais wa nchi na kutekeleza.

Kuhusu vita vya dawa za kulevya Waziri wa Katiba na Sheria MWAKYEMBE amesema ni vigumu na vinahitaji ushirikiano wa watu wote kwani ni biashara ya kimtandao.

Dakta MWAKYEMBE ametoa ufafanuzi huo kufuatia kuwepo kwa malalamiko kuwawakuu wa mikoa wana madaraka makubwa na hata kuweza kuwasimamisha kazi watumishi wenzao.

No comments