Marekani yaiwekea Iran vikwazo
Marekani yaiwekea Iran vikwazo
Utawala wa Rais wa Marekani Donald Trump umeiwekea vikwazo Iran kufuati hatua yake ya hivi majuzi ya kulifanyia jaribio kombora.
Wizara ya fedha ya Marekani ilitangaza hatua dhidi ya watu 13 na kwa kampuni kadha leo Ijumaa.
Rais Donald Trump aliandika mapema kwenye mtandao wa twitter kuwa,"Iran inacheza na moto, hawana shukran jinsi Obama alikuwa mkarinu kwao, Si mimi!"
Lakini Iran inasema kuwa hauwezi kulegeza kamba kutokana na vitisho visivyo na maana vya Marekani, kutoka kwa mtu asiye na juzi Iran yajaribu kombora la nyuklia
Kati ya makudi yaliyowekewa vikwazo yako nchi ya miliki za kiarabu , Lebanon na China.
Wiki hii mshauri wa masuala ya ulinzi Michael Flynn, alisema kuwa Marekani inaionya Iran kufuatia jaribio hilo la kombora.
Lakini waziri wa mashauri ya nchi za kigeni kwa Iran Mohammad Javad Zarif, leo Ijumaa aliandika kwenyr mtandao wa twitter akisema kuwa Jamhuri hiyo ya kiislamu haitikizwi na vitisho vya Marekani.
Alisema kuwa Iran haina mapango yoyote ya kutumia jeshi lake dhidi ya nchi yoyote bali kujilinda.
mtuwangu wanguvu angalia video ya mtoto wakichina akiendesha katapila
Post a Comment