Mkuu wa Wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza amekabidhi Kituo cha Radio
Mkuu wa Wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza Bw. Emmanuel Kipole amekabidhi Kituo cha Radio Sengerema kwa Halmashauri ya Wilaya ya Sengeremakwa ajili ya kuratibu kituo hicho.
Bw. Kipole alikabidhi kituo hicho Februari 9, mwaka huu (jana) katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema, ambapo alihudhuria Kikao cha Madiwani wa Halmashauri hiyo.
Alisema kuwa kituo hicho ni mali ya wananchi kutokana na michango iliyotolewa na halmashauri na pia kupitia wahisani mbalimbali.
Hata hivyo toka kuanzishwa kwa Radio Sengerema Serikali ya Halmashauri ya Wilaya hiyo haikukisimamia, ambapo walijitokeza baadhi ya wananchi kwa ajiliya kutoa kero amabazo zipo kwenye redio hiyo
Post a Comment