Manchester City imeichapa Bournemouth kwa mabao 2-0
Manchester City imeichapa Bournemouth kwa mabao 2-0 katika mchezo wa Ligi Kuu ya England na kurejea katika nafasi ya pili kwenye msimamo.
Bournemouth walijaribu kufurukuta na kuzuia mashambulio ya City, lakini hawakuweza kuiteteresha ngome ya City. Goli la pili la City lilikuwa la kujifunga kupitia Tyrone Mings katika dakika ya 69.
Man City sasa imefikisha pointi 52, nane nyuma ya Chelsea wanaoongoza ligi wakiwa na pointi 60. Hata hivyo ushindi wa Man City huenda ukawa umeingia chachu kidogo, kufuatia Gabriel Jesus kuumia.
Post a Comment