Wizara ya Nishati na Madini yaanza kuhamia DODOMA
Baadhi ya Wafanyakazi wa Wizara ya Nishati na Madini leo wameondoka rasmi Jijini DSM kuelekea mkoani DODOMA ikiwa ni hatua ya utekelezaji wa agizo la Rais JOHN MAGUFULI la kutaka wizara zote kuhamia mkoani humo.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini JULIANA PALLANGYO
Baadhi ya Wafanyakazi wa Wizara ya Nishati na Madini leo wameondoka rasmi Jijini DSM kuelekea mkoani DODOMA ikiwa ni hatua ya utekelezaji wa agizo la Rais JOHN MAGUFULI la kutaka wizara zote kuhamia mkoani humo.
Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo JULIANA PALLANGYO amesema kuwa hii ni awamu ya kwanza ya utekelezaji wa agizo hilo.
PALLANGYO pia amewapongeza wafanyakazi wote waliokubali kuhamia mkoani DODOMA bila malalamiko na kuahidi kuwa shughuli zote za kikazi zitaendelea kama kawaida.
Hatua ya wizara mbalimbali kuhamishia ofisi zake mkoani DODOMA inafuatia agizo lililotolewa mwaka 2016 na Rais JOHN MAGUFULI la kuzitaka Wizara zote kuhamia mkoani humo mpaka ifikapo februari 28 mwaka huu.
Post a Comment