Wadau wa kilimo na uvuvi watakiwa kujifunza
Wadau wa kilimo na uvuvi watakiwa kujifunza
Mkurugenzi
Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi, Eliurd Mwaiteleke amewataka wadau
wa kilimo na Uvuvi kutumia vyema fursa
za Maendeleo ya Sekta ya Kilimo na
Mifugo zinazotolewa na taasisi za umma zilizopo wilayani hapo.
Mwaiteleke
alisema hayo wakati wa ziara katika Kituo
cha Utafiti wa Kilimo cha Ukiriguru, Chuo cha Mafunzo ya Kilimo Ukiriguru,
Shamba la Uzalishaji wa Mifugo la Mabuki, Kituo cha Utafiti wa Mifugo Mabuki
pamoja na Chuo cha Mafunzo ya Mifugo Mabuki.
Kwa
upande wake, Kaimu Afisa Habari na Mawasiliano katika Halmashauri ya Wilaya ya
Misungwi, Thomas Lutego alieleza
vipaumbele vya halmashauri katika juhudi za kukuza uchumi ambapo ni pamoja kufufua kilimo cha zao la pamba
na kuanzisha kilimo cha zao la alizeti
ikiwa ni zao la biashara pamoja na kusindika mafuta yatokanayo na zao hilo.
Lutego
alisema kuwa halmahsuri itatoa mbegu za alizeti
kwa kuwakopesha wakulima, ambapo tayari Maafisa Ugani na Watendaji wa Kata na
Vijiji wanaendelea na utoaji wa elimu kwa wakulima na kuwaorodhesha ili kupata
takwimu halisi ya mahitaji kwa msimu huu.
Kaimu Mkurugenzi wa
Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Ukiriguru, Everine Lukonge alisema wameweza
kubaini vipengele mbalimbali vya kuongeza thamani ya mazao ikiwemo zao la pamba, mihogo, ulezi, mtama, mbaazi, dengu, karanga
na alizeti ambapo yanafaa kwa asili ya udongo katika Wilaya ya hiyo.
Lukonge alisema
kwamba vijiji vilivyofanyiwa utafiti na
kufanikiwa kulima vizuri katika zao la dengu katika Kijiji cha Iteja na Ilalambogo, mtama na uwele
na kulimwa katika Vijiji vya Ng’ombe na Mapilinga.
IMEANDIKWA NA MWANDISHI WA KALI ZOTE BLOG James Timber, Misungwi KUTOKA
Post a Comment