Header Ads

Kamanda sirro awaita waliotajwa na Makonda


Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam amewataka watu wote waliotajwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kuhusika na dawa za kulevya, kuripoti kituo kikuu cha polisi kama walivyoamrishwa na mkuu huyo wa mkoa.

Kamanda Sirro ameema leo ndiyo siku ambayo walitakiwa kuripoti kituoni hapo, lakini hadi majira ya saa 7 mchana walikuwa ni watu wanne pekee ambao walikuwa wamekwisha ripoti tofauti na wale wawili walioripoti jana.
Kati ya walioripoti siku ya leo yumo aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Kinondoni Idd Azzan huku akisita kuwataja wengine, ikiwa ni tofauti na wawili walioripoti jana akiwemo Mchungaji Josephat Gwajima.
Sirro amesema wawili hao walioripoti jana wanaendelea kushikiliwa na polisi kwa mahojiano zaidi juu ya kuhusishwa na dawa za kulevya.
Idd Azzani
Wakati Kamanda Sirro akisisitiza watu hao kuripoti kituoni, Mbunge wa Hai Freeman Mbowe ambaye ni mmoja kati ya watu waliotajwa, akiwa mjini Dodoma amekanusha kuhusika na dawa za kulevya, huku akilitaka jeshi la polisi kuata taratibu za kisheria za kumuita kituoni hapo badala ya njia iliyotumika
Sikiliza hapa sehemu ya alichokizungumza Mbowe siku ya leo

No comments