Header Ads

Rama Dee amkosoa Makonda

Msanii wa muziki wa bongo fleva Rama Dee amefunguka na kusema kuwa yeye hamuungi mkono Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kwa namna anavyoshugulika na kuwafikisha polisi baadhi ya wasanii wanaotuhumiwa kuhusika na dawa za kulevya.





Rama Dee anasema Paul Makonda ni kiongozi mzuri ila siku zote huwa anafanya vitu kwa haraka bila kushirikisha baadhi ya viongozi ambao wapo kwenye uongozi kwa muda mrefu na kusema yeye haungi mkono kitendo cha baadhi ya wasanii kuwekwa ndani ila angemuunga mkono kwa kuziba mirija ya wauzaji wakubwa wa madawa ya kulevya.
"Makonda ni kiongozi mzuri sana Ila ana maamuzi ya haraka bila kushirikisha watu wenye experiences na uongozi, mimi kama msanii, siungi mkono wasanii kuwekwa ndani ila ningemuunga mkono kama angeweza kuziba mirija ya wauzaji Papa kuwafikia wasanii na watanzania kwa ujumla. Tangu nipo mdogo wauza unga wanafahamika na majina yao yapo kwenye mitandao lakini sijawahi ona wakikamatwa wala kuoneshwa kwenye vyombo vya habari! Hata hao polisi pia sijaona picha zao" alisema Rama Dee 
Mbali na hilo Rama Dee amesema kuwakamata baadhi ya watu kwa kuhisi, si jambo zuri kwani jambo hilo linaweza kuleta madhara makubwa na kuharibu maisha ya watu kuliko hata hizo dawa za kulevya.
Paul Makonda
"Wasanii ni watu kama watu wengine tu hivyo unapoanza kuharibu biashara zao kwa sababu tu upo na power ya uongozi sidhani kama ni busara, unajua haya mambo unaweza ona ya kawaida ila yanaweza kuharibu maisha ya watu kuliko hata huo unga! hasa wasanii".
Ameendelea kusema "Namuunga mkono Nape kuwa kuna njia za kutumia ambazo zinalinda sheria ya mtuhumiwa! Ila ukitumia nguvu bila akili ni sehemu mojawapo ya kuwapatia pesa wanasheria bila msingi wowote. Kukamata watu kwa kuhisi, ni utaratibu mbaya sana,kumbuka kuna watu wapo na chuki za maendeleo ya watu wengine unaweza ukasikia hata Tale anauza unga ambaye ni rafiki yako, sijui utafanyaje hapo" Alisema Rama Dee 

Wema Sepetu alipokuwa akiwasili kituo cha Polisi kwa mahojiano

No comments