Arsene Wenger: asema bado atakuwa kazi msimu ujao
Meneja wa Arsenal Arsene Wenger amesema kwamba hana shaka yoyote kwamba atakuwa bado anafanya kazi ya umeneja msimu ujao, Arsenal au "kwingineko".
Wenger, 67, alikuwa akiongea baada ya moja ya wiki mbaya zaidi kwake katika miongo miwili ambayo amekuwa Arsenal.
Baada ya kichapo cha 5-1 mikononi mwa Bayern Munich Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya Jumatano, wachezaji kadha wa zamani walisema wanaamini muda wake Emirates unakaribia kikomo.
Mkataba wa Mfaransa huyo unamalizika mwishoni mwa msimu.
Wenger amesema ataamua kuhusu mkataba mpya Machi au Aprili.
"Bila kujali yatakayotokea, nitakuwa meneja msimu mwingine. Hata kama ni hapa au kwingineko, hilo nina uhakika nalo," Wenger alisema Ijumaa.
"Iwapo nilisema Machi au Aprili, ni kwa sababu sijui. Sitaki kusema kisha nibadili msimamo.
"Nimzoea kukosolewa. Maishani ni muhimu kufanya lile unalofikiria kwamba ni sahihi na hayo mengine kuwaachia wengine. Ninafanya kazi ya umma na lazima nikubali kukosolewa, lakini ni sharti pia nifuate maadili yangu."
Vikombe walivyoshinda Arsenal chini ya Wenger
Ligi ya Premia (3) | 1997-98, 2001-02, 2003-04 |
Kombe la FA (6) | 1997-98, 2001-02, 2002-03, 2004-05, 2013-14, 2014-15 |
Ngao ya Jamii (6) | 1998, 1999, 2002, 2004, 2014, 2015 |
Gunners watasafiri kwa Sutton United Jumatatu kwa mechi ya Kombe la FA
Post a Comment