Shirika la viwango nchini TBS wametengeneza jumla ya viwango 300
Shirika la viwango nchini TBS wametengeneza jumla ya viwango 300 kwa mwaka wa Fedha wa 2016/2017 vitakavyoanza kutumika kupima ubora wa bidhaa katika sekta mbalimbali za uzalishaji ili kukuza Viwanda hapa nchini
Kaimu mkurugenzi wa TBS Profesa EGIDI MABOFU amesema kati viwango vilivyotengenezwa jumla ya viwango 75 zimeshathibitishwa na waziri wa biashara viwanda, na uwekezaji na vimeshaanza kutumika.
Kuhusu kuwepo kwa bidhaa hafifu sokoni MABOFU amesema TBS imeendelea kuimarisha ukaguzi wa bidhaa zinazotoka nje ili kuhakikisha zinaingia bidhaa zenye viwango bora na ambazo hazitaua Soko la Viwanda vya ndani.
chanzo tbc
Post a Comment