Header Ads

askari 9 wanaotuhumiwa kushirikiana na wafanya biashara ya madawa ya kulevya.


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amewataja askari 9 wanaotuhumiwa kushirikiana na wafanya biashara
Aidha amewataja wasanii wanaojihusisha na matumizi na uuzaji wa Madawa ya kulevya na kuwataka kuripoti kituo cha polisi kesho.
Akiongea na waandishi wa habari akiwa ofisini kwake Alhamisi hii, RC Makonda amewataka wauzaji wote kufika makao makuu ya polisi kwajili ya kujieleza.
“Nimeamua kuingia kwenye hii vita kwa sababu najua siku moja Mungu ataniuliza, nilikupa mkoa wa Dar es salaam kupitia Rais John Pombe Magufuli watoto waliangamia kwa Madawa ya kulevya, sitaki kufika mbungini nisiwe na jibu, nipo tayari kupoteza ukuu wangu wa mkoa, nipo tayari kutangulia kwa aliyeniumba lakini niwe na jibu kwa mungu wangu aliyeniumba kwamba Madawa ya kulevya hayakubaliki ndani ya Dar es salaam,” alisema Makonda.
Aliongeza,’Wapo tuliowakamata pamoja na dawa zao tumeshawafikisha Central Polisi na wanaendelea na mambo yanayotakiwa. Lakini wapo ambao bado, majina ni mengi sana mtayapitia wenyewe, kuna Mchafu, Director Joan, Mirror, Rommy na wengine wengi, wapo wauzaji wadogo na wengine wakubwa. Lakini wapo wengine wanasemekana wanatumia lakini hakuna ushahidi kwamba wanatumia ingiwa wenzao wanasema wanatumia, ni bora nikakutana nao kesho pale Central, akiwemo TID, Wema Sepetu,”





No comments