CHAMA cha Waandishi wa Habari wa Kupiga Vita Matumizi ya Dawa za Kulevya
CHAMA cha Waandishi wa Habari wa Kupiga Vita Matumizi ya Dawa za Kulevya
CHAMA cha Waandishi wa Habari wa Kupiga Vita Matumizi ya Dawa za Kulevya na Uhalifu Tanzania (OJADACT) kimeunga mkono hatua zilizochukuliwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda katika vita dhidi ya madawa ya kulevya.
Juzi akizungumza na wanahabari, Makonda alitaja majina ya wasanii wakubwa wanaodaiwa kutumia dawa hizo pamoja na kuagiza kukamatwa kwa polisi tisa walioko kwenye mtandao wa usambazaji wa dawa za kulevya jijini humo.
Mwenyekiti wa OJADACT, Edwin Soko ametoa msimamo huo jana jijini Mwanza wakati akizungumza na wanahabari ambapo alisema hatua hiyo ni muhimu katika vita dhidi ya matumizi ya dawa za kulevya kwani jiji hilo limekuwa kitovu cha uingizaji na usafirishaji wa dawa hizo.
“Biashara ya dawa za kulevya hazistaili kufumbiwa macho kwa sababu zina athari kubwa kwa jamii ikiwemo kuuathili mwili kiroho na kiakili ambapo madhara hayo hutokana na utumia aji wa dawa hizo na endapo yakiachwa yaendelee yanaweza kukwamisha ustawi wa taifa kuekea kwenye uchumi wa viwanda.
“Tunapongeza kitendo hicho cha viongozi wetu kufikia hatua ya kuyataja hadharani majina ya wauzaji wa dawa za kulevya kwasababu jambo hili siyo rahisi na haikuwezekana huko nyuma kwahiyo kutokana na hili ni vyema wakuu wa mikoa mingine waanze kuchukua tahadhari ya kupambana na watu watakaohamia mikoani baada ya kutangaziwa vita jijini Dar es Salaam, kwahiyo Mwanza, Tanga, Arusha nao wajipange kupambana na wafanyabiashara hawa,” alisema.
Akizungumzia kuhusu hali ya dawa za kulevya nchini, Soko alisema hali siyo nzuri kwani kuna ongezeko kubwa la matumizi ya dawa za hizo na kuitaka jamii kushiriki kwa kuwaumbua wauzaji na wasambazaji kwasababu wanaishi katika jamii na siyo suala hilo kuiachia serikali pekee.
“Matumizi ya Bangi yameongezeka kwa asilimia 6.5 kwa mwaka 2015/16 ambapo watumiaji 247 walishikiliwa kwa tuhuma hizo na matumizi ya dawa za viwandani aina ya Heroine na Cocaine nayo yameongezeka,” alisema.
OJADACT wanasisitiza kwamba ni muhimu haki itendeke katika kuwashughulikia watakaopatikana na hatia katika sakata hilo na biashara ya dawa za kulevya kiujumla kadri sheria ya kuthibiti dawa za kulevya ya mwaka 2015 inavyosema.
imeandikwa na mwandishi wetu wa KALIZOTE BLOG Na James Timber KUTOKA Mwanza
Post a Comment