weusi atuna tatizo na msanii yoyote
Msanii wa muziki wa hip hop, Joh Makini amefunguka na kusema kuwa wao kama Weusi hawashindani na msanii yoyote yule ila wao wanafanya muziki katika kutimiza ndoto zao.
Weusi
Joh Makini alisema Weusi wanafanya muziki ili kutangaza nchi, kutimiza ndoto zao katika maisha na si kushindana na msanii yoyote yule.
“Watu kwanza wanatakiwa wajue sisi hatushindani na mtu yeyote kwenye muziki huu watu wasichanganye vitu, sisi tupo hapa kwa ajili ya kutengeneza ndoto zetu, kuendesha maisha yetu na kuitangaza nchi yetu Tanzania kupitia hiki ambacho ametubariki” alisema Joh Makini
Post a Comment