Header Ads

AGAPE LA WAPA MBINU WATOTO WA KIKE MKOANI SHINYANGA

                                                
Baadhi ya watoto waliokolewa katika ndoa na mimba za utotoni  na shirika la Agape la mjini shinyanga  ameelezea namna shirika hilo lililivyowawezesha kuapata ujunzi katika fani mbalimbali ili waweze kujiajiri.

Image result for PICHA ZA WANAFUNZI WA CHUO KIKUU
COPY  MTANDAONI

Wakizungumza katika chuo cha maendeleo ya wananchi (FDC) kilichopo Buhangija mjini Shinyanga wasichana hao wameeleza kuwa shirika hilo baada ya kuwatoa katika mazingira magumu waliyokuwa wakiishi  limewapeleka katika chuo hicho na kupata ujuzi katika fani mbalimabali ambao ni pamoja na ushonaji wa nguo na umeme.


Wamesema ujuzi huo walioupata utawasaidia kujiari na kuendesha maisha yao tofauti na hapo awali ambapo walikuwa wamekata tama.

Kwa upande wake mwalimi wa somo la ushonaji  katika chuo hicho Rebeka  Maningu  ameeleza kufurahioshwa kwake na shirika la AGAPE kwa hatua linazochukua katika kumkomboa mtoto wa kike.

Shirika la AGAPE ambalo linajihusisha na utetezi wa haki za wanawake na watoto ni kwa muda mrefu linaendesha kampeni maaalum ya kuzuia tatizo la ndoa na mimba za utotoni

No comments