Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dkt. Islam Seif amesema kuwa kuanzishwa kwa sera ya kusimamia bahari kuu kutasaidia kuondoa tatizo la uvuvi haramu nchini
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dkt. Islam Seif amesema kuwa kuanzishwa kwa sera ya kusimamia bahari kuu kutasaidia kuondoa tatizo la uvuvi haramu nchini.
Dkt. Islam Seif amesema kuwa sera hiyo imelenga kuikuza sekta ya uvuvi wa bahari kuu ambayo ikitumika ipasavyo itasadiai kuinua uchumi wa nchi kwa kiasi kikubwa kupitia sekta hiyo ya Uvuvi.
Dkt. Seif amebainisha hayo wakati akifungua mkutano wa kujadili rasimu ya sera ya kusimamia uvuvi katika bahari kuu iliyofanyika mjini Unguja viwasini humo na kuongeza kuwa rasimu hiyo itaimairsha uwezo wa fedha na miundombinu kwa mamlaka hiyo ili kuboresha utendaji.
Amesema sera hiyo imezingatia hasa ushirikishwaji wa wazawa utahakikisha upatikanaji wa ajira kwa wananchi na pia itaweza kuboresha sekta ya viwanda ambayo ndiyo tegemeo la ukuaji wa uchumi wa nchi kwa sasa.
Post a Comment