Kampuni ya Apple imeripoti kushuka kwa mapato yake ya mwaka kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2001.
Kampuni ya Apple
imeripoti kushuka kwa mapato yake ya mwaka kwa mara ya kwanza tangu
mwaka 2001. Matokeo ya robo ya mwisho ya mwaka wa fedha nchini Marekani
imethibitisha mwenendo wa robo mbili zilizopita kuwa mapato yalishuka
kwa asilimia tisa.
Wachambuzi wanasema kuwa ni dalili ya kuwepo kwa bidhaa nyingi za simu sokoni.
Robo ya mwisho inaisha muda mfupi baada ya kuongezeka kwa iphone 7, kunamaanisha kuwa matokeo ya mauzo katika bidhaa mpya hazitoshelezi katika takwimu za hivi karibuni.
Post a Comment