Michuano ya Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara inatarajiwa kuendelea tena hapo kesho katika mzunguko wake wa 13 kwa michezo mitano kupigwa katika viwanja mbalimbali hapa nchini
Michuano ya Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara inatarajiwa kuendelea tena hapo kesho katika mzunguko wake wa 13 kwa michezo mitano kupigwa katika viwanja mbalimbali hapa nchini
Mkurugenzi wa benchi la ufundi wa African Lyon Charles Otieno amesema, Prisons ina wachezaji wazuri ambao wanapambana kuhakikisha wanapata pointi tatu kwa kila mchezo lakini kwa upande wao wamejipanga ikiwa ni pamoja na kurekebisha makosa yaliyokuwa yakijitokeza katika michezo iliyopita.
Kwa upande wake nahodha wa Tanzania Prisons Laurian Mpalile amesema, wamejipanga kwa ajili ya kuweza kupambana ili kubaki katika nafasi nzuri ndani ya ligi kwani kikosi kimeanza kuwa katika hali nzuri na kinazidi kupambana ili kujihakikishia kinafikia malengo mpaka mzunguko wa kwanza wa Ligi unapokamilika.
Michezo mingine itakayopigwa hapo kesho ni Toto Africans dhidi ya Mtibwa Sugar katika Uwanja wa CCM Kirumba, Mbeya City itakuwa mwenyeji wa Majimaji katika Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya, Mwadui FC ya Shinyanga itaikaribisha Simba katika Uwanja wa CCM Kambarage mkoani Shinyanga wakati JKT Ruvu itaikaribisha Ndanda kwenye Uwanja wa Mabatini.
Jumapili Yanga watawakaribisha Mbao FC katika Uwanja wa Uhuru wakati Ruvu Shooting ikiwa mwenyeji wa Stand United kwenye Uwanja wa Mabatini mkoani Pwani.
Post a Comment