Header Ads

Tanzania KUKUWA KIUCHUMI

Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amesema ujio wa Mfalme wa Morocco nchini Tanzania ni fursa kubwa ya kibiashara na uwekezaji kwa Tanzania na Morocco ambapo Tanzania imesaini mikataba 21 ya ushirikiano baina ya nchi hizo mbili.


Rais Dkt. Magufuli ameyasema hayo leo Ikulu jijini Dar es Salaam wakati wa ziara ya Mfalme wa Morocco Mohammed VI ambapo amesema Tanzania ni eneo zuri la uwekezaji pamoja na kuainisha mambo mbalimbali katika mazungumzo yao ikiwemo uwekezaji katika sekta mbalimbali nchini, utakaosaidia kukuza pato la taifa.
Akitaja baadhi ya makubaliano, Rais Magufuli amekuwa kuwa ni pamoja Mfalme Mohamed VI kuihakikishia nchi kuwa kutakuwa na ndege ya moja kwa moja kutoka Rabat Morocco hadi Dar es Salaam Tanzania, kutolewa kwa nafasi kwa askari wa Tanzania takribani 150 watakaokwenda kujifunza masuala ya ulinzi na usalama nchini Morocco.
Rais Dkt. John Magufuli amesema amemuomba Mfalme  huyo kuijengea Tanzania Msikiti Mkubwa Jijini Dar es salaam na uwanja mkubwa wa mpira mkoani Dodoma jambo ambalo amekubali.
“Nimemuomba Mfalme atujengee uwanja mkubwa wa mpira mkoani Dodoma na Msikiti mkubwa Jijini Dar es salaam jambo ambalo amekubali kitu ambacho kitazidi kuongeza uhusiano wetu kati ya nchi hizi mbili” Amesema Rais Magufuli.
Aidha Rais amewataka wafanyabiashara wa Tanzania kuchangamkia furasa za kibiashara zilizopo Comoyro na ambazo zipo nchini katika kupeleka Comorro ili kuhakikisha kwamba uchumi wa Tanzania unakuwa.
Mfalme wa Morocco yupo nchini kwa ziara ya kikazi ya siku tatu ambapo kwa mujibu wa Rais Dkt. Magufuli ameongeza siku moja kuwepo nchini .
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Mtukufu Mfalme wa Morocco Mohamed VI wakilakiwa na wafanyakazi pamoja na wageni mbalimbali katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam mara baada ya kuwasili.

No comments