Header Ads

Katika kuadhimisha miaka mitano tangu kuanza kwa kipindi chake cha runinga, The Mboni Show, Mboni Masimba amekuja na kongamano liitwalo ‘Sauti ya Mwanamke.

Katika kuadhimisha miaka mitano tangu kuanza kwa kipindi chake cha runinga, The Mboni Show, Mboni Masimba amekuja na kongamano liitwalo ‘Sauti ya Mwanamke.

14676781_1781677918716385_2459758754313273344_n
Akiongea na Bongo5, Mboni amesema kongamano hilo litafanyika katika mikoa mbalimbali nchini na November 6 litaanza kwa kufanyika jijini Mwanza. Amesema kuwa hiyo ni sehemu ya ahadi yake ya kurudisha kwa jamii.
Amesema imeandaliwa kwaajili ya wanawake ili kuwapa elimu na mafunzo ya fani mbalimbali kutoka kwa wanawake wenzao na dhamira kuu ikiwa kuwafanya watambue umuhimu wao na kujikwamua kiuchumi.
“Wanawake wengi hawana uthubutu, wanawake wengi ni waoga. Kwahiyo Sauti ya Mwanamke itaweza kuzunguka nchi nzima kuweza kumwezesha mwanamke kupaza sauti yake,” amesema Mboni.
Amesisitiza kuwa watoa mada kwenye kongamano hilo wote watakuwa wanawake.
Sauti ya Mwanamke itafanyika kwenye ukumbi wa Gold Crest huku kiingilio kikiwa ni shilingi 40,000.

CHANZO BONGO 5

No comments