Header Ads

Msanii wa vichekesho nchini Kingwendu amesema mambo ya siasa yalimsababisha kupunguza kazi zake za sanaa



Msanii wa vichekesho nchini Kingwendu amesema mambo ya siasa yalimsababisha kupunguza kazi zake za sanaa kwa kuwa alikuwa katika kujipigia kampeni za kugombea ubunge. 
Kingwendu

Pia Kingwendu amesema kama angefanikiwa kupata ubunge angeweka mambo ya sanaa pembeni kidogo kwa kuwa siasa ina mambo mengi na inabidi ujipe muda wa kutosha ili kuweza kukamilisha majukumu yako vizuri.

Hata hivyo Kingwendu amesema “unajua Alikiba na Diamond wapo juu kwa sababu wanapata promo na hata mimi nikipata promo ya kutosha nitarudi na nitashaini kama zamani kwa hiyo naombeni wadau mnibebe jamani” alisema Kingwendu.

No comments