Jeshi la Polisi kupitia kikosi kazi maalum cha mkoa wa Dar es Salaam kwa kushirikiana na kikosi maalum cha kupambana na uhalifu mkoa wa Pwani limefanikiwa kuwaua watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi katika kijiji cha Mtambani wilayani Mkuranga.
Jeshi la Polisi kupitia
kikosi kazi maalum cha mkoa wa Dar es Salaam kwa kushirikiana na kikosi
maalum cha kupambana na uhalifu mkoa wa Pwani limefanikiwa kuwaua watu
wanaosadikiwa kuwa ni majambazi katika kijiji cha Mtambani wilayani
Mkuranga.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Gilles Muroto
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Temeke, SACP Gilles Muroto ametoa taarifa hiyo leo, na kusema kuwa tukio hilo limetokea Oktoba 21 mwaka huu majira ya saa 5 usiku katika mapambano ya askari wa kikosi hicho na watu hao, baada ya askari hao kuzingira nyumba waliyokuwemo, na kuanza kurushiana risasi.
Kamanda Muroto amesema pia kuwa katika tukio hilo askari mmoja kwa kikosi hicho alijeruhiwa bega na kulazwa Muhimbili kwa matibabu, huku watuhumiwa wengine zaidi ya watano wakitoroka.
Amesema mbali na kuwaua majambazi wanne, pia walikamata bunduki moja aina ya shortgun pump na risasi zaidi ya 11.
Kwa mujibu wa Kamanda Muroto, watu hao wana umri wa kati ya miaka 25 na 30 na waliouawa miili yao imehifadhiwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili huku likiendelea kuwasaka waliotoroka.
Jeshi hilo limesema linaendelea kufanya msako wa majambazi na kuwataka wananchi kutoa ushirikiano kwa kutoa taarifa pindi wanapoona dalili zisizoeleweka.
Post a Comment