Header Ads

Azam FC KUJIANDA KUZICHAPA NA Kagera Sugar

Kikosi cha Azam FC, kimeondoka leo kuelekea mkoani Kagera kuwafuata Kagera Sugar kwa ajili ya muendelezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara, mchezo utakaopigwa Oktoba 28 katika Uwanja wa Kaitaba.


Azam FC imeondoka huku ikiwa na kumbukumbu ya kushinda bao 1-0 katika mchezo wake         dhidi ya JKT Ruvu uliopigwa Jumamosi ya Oktoba 22 katika Uwanja wa Chamazi Complex.
Kikosi kilichosafiri kinaundwa na jumla ya wachezaji 22, ambao ni:- 
Makipa: Aishi Manula, Mwadini Ally na Metacha Mnata.
Mabeki: Shomary Kapombe, Aggrey Morris, Daniel Amoah, Erasto Nyoni, David Mwantika,            Gadiel Michael, Ismail Gambo.
Viungo: Himid Mao, Salum Abubakar, Frank Domayo, Jean Mugiraneza, Mudathir Yahya,                 Ramadhan Singano, Bruce Kangwa, Khamis Mcha, Masoud Abdallah.
Washambuliaji: John Bocco (C), Francisco Zekumbawira, Gonazo Bi Ya Thomas Renardo,         Shaaban Idd.

No comments