VIDEO YA WATOTO WAKICHINA WAKIPANDA MLIMA WA MITA 800
Huko China kitongoji cha Sichuan, kwa muda mrefu watoto wamekuwa wakishuka na kupanda mita 800 za mlima kila siku kwenda na kurudi shule kwa kutumia njia za kienyeji ambazo ni ngazi za miti.
Kwa sasa wakazi wa kijiji hicho wameanza mchakato wa kujenga ngazi ya chuma mradi unaotarajiwa kukamilika mwezi November mwaka huu.
Ngazi hiyo ambayo inatarajiwa kuwa na muundo imara zaidi na salama itarahisishia maisha ya wanakijiji hao ambao wamekuwa wanaitumia ngazi hiyo kupanda na kushuka kila wiki kununua bidhaa mbalimbali na kufanya biashara zao katika soko ambalo liko mbali na wanakoish
Post a Comment