Header Ads

Korea kaskazini inadai kupiga hatua katika mradi wake wa kutengeneza silaha za nyuklia licha ya upinzani wa kimataifa na vikwazo vikali.


Waangalizi wanasema Korea kaskazini wamepiga hatua katika kutengeneza makomboraImage copyrightKCNA
Image captionWaangalizi wanasema Korea kaskazini wamepiga hatua katika kutengeneza makombora
Sera ya Marekani kuishawishi Korea kaskazini kuachana na mpango wake wa kutengeneza silaha za nyuklia huenda 'haina ufanisi' , mkurugenzi wa shirika la kitaifa la ujasusi Marekani amesema.
James Clapper amesema Marekani jambo ambalo Marekani inaweza kutumainia ni kuzuia uwezo wa taifa hilo, katika hotuba New York.
Ni nadra kwa Marekanikukiri kuwa lengo lake kuu la kuwa na dunia isiyokuwana matumizi ya nyuklia huedna isifanikiwe.
Hatahivyo, wizara ya mambo ya nje Marekani inasema sera yake hiyo haijabadilika.
Korea kaskazini inadai kupiga hatua katika mradi wake wa kutengeneza silaha za nyuklia licha ya upinzani wa kimataifa na vikwazo vikali.
Mnamo Septemba, ilifanya jaribio lake la tano na kubwa la silaha zake za nyuklia, jambo lililozusha shtuma kote duniani.
Akizunguma katika baraza kuhusu uhusiano wa nchi za nje siku ya Jumanne, Clapper ameitaja serikali ya KOrea  kama iliyo na 'uoga' na kusema inaona silaha za nyuklia kama 'tikiti yao ya kuendelea kuwepo'.
Amependekeza, kutoa vikwazo vya kiuchumi kwa kiongozi wa Korea kaskazini Kim Jong-un kupunguza silaha zake za nyuklia 
chanzo bbc

No comments