Maua Sama UTAJILI MALANGONI
Baada ya So Crazy, licha ya kufanya vizuri sana kwenye redio, ilikuwa si rahisi kuona kuwa muziki utaanza kumlipa Maua Sama katika kipindi kifupi. Hiyo pia ilichangiwa na yeye kuwa masomoni Moshi, Kilimanjaro na hivyo kukosa muda wa kuusimamia muziki wake vyema.
Mambo yamebadilika. Baada ya kumaliza chuo na kuhamia Dar es Salaam kuanza kuutafuta mkate wake wa kila siku kupitia muziki. Mungu si Athumani, baada ya kuachia hit single zake mbili, Mahaba Niue na Sisikii, muimbaji huyo mwenye sauti tamu, ameanza kuyaona matunda ya jitihada zake.
“Mahaba Niue na Sisikii ni nyimbo ambazo zimebadilisha maisha yangu,” Maua alimwambia mtangazaji wa kipindi cha Supa Mega cha Kings FM, Prince Ramalove.
“Kama msanii zilinifanya nijulikane zaidi, kimapato, mwelekeo wa muziki wangu pia umeonekana tayari sababu ya hizo nyimbo mbili,” aliongeza.
Kwa sasa Maua Sama aliyevumbuliwa na Mwana FA, anawekwa kwenye orodha ya wasanii wa kike wanaofanya vizuri Tanzania.
Post a Comment