Header Ads

Kocha wa Mbeya City Kinnah Phiri amesema, amekipanga kikosi chake vizuri kwa ajili ya kuweza kuvuna pointi tatu



Kocha wa Mbeya City Kinnah Phiri amesema, amekipanga kikosi chake vizuri kwa ajili ya kuweza kuvuna pointi tatu hapo kesho katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam dhidi ya African Lyon ikiwa ni muendelezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara.
 

Akizungumza mara baada ya kumaliza mazoezi ya maandalizi ya mchezo wa kesho, Phiri amesema, anawaamini vijana wake japo wamepoteza baadhi ya michezo lakini anaamini watazingatia yale yote aliyowafundisha ili kuweza kuwapa furaha mashabiki wa jijini Mbeya.

Kwa upande wake dakta wa Mbeya City Joshua Kaseko amesema katika mchezo wa kesho watamkosa mshambuliaji Omary Ramadhani ambaye ni mgonjwa huku kiungo mshambuliaji Joseph Maundi akiendelea kuangalia hali yake kama itaruhusu kucheza kutokana na majeraha aliyoyapata huku akiongeza kuwa kikosi kipo katika hali nzuri na wamepunguza uchovu kwa wachezaji hapo jana kwa kutumia njia za kisayansi.

Mbeya City inaingia kupambana na African Lyon hapo kesho huku ikiwa na kumbukumbu ya kutoa sare katika mchezo wao dhidi ya Ndanda FC uliopigwa Jumatano ya wiki hii katika Uwanja wa Nangwanda Sijaona Mjini Mtwara huku African Lyon ikiwa na kumbukumbu mbaya ya kuchapwa kwa mabao 2-0 na timu ya Majimaji katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam.

No comments