Header Ads

Serikali imepanga kuingiza nchini mitambo ya kusindika maziwa na bidhaa zitokanazo na maziwa



Serikali imepanga kuingiza nchini mitambo ya kusindika maziwa na bidhaa zitokanazo na maziwa, kwa ajili ya vikundi vya wajasiriamali na wakulima wanaojihusisha na biashara ya ufugaji, ikiwa ni hatua ya kuelekea ujenzi wa uchumi wa viwanda. 
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mh. Charles Mwijage ametoa ahadi hiyo jijini Dar es Salaam leo, na kusema kuwa kwa kuwapatia wakulima mitambo hiyo, serikali itakuwa inatekeleza kwa vitendo sera ya ujenzi wa viwanda ambayo ndiyo itakayoifikisha Tanzania kuwa taifa la uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.

Amefafanua kuwa sera ya ujenzi wa viwanda itafanikiwa kupitia uendelezaji wa viwanda vidogo vidogo na kutolea mfano wa nchi za China, Japan, Marekani, India, Indonesia na Malaysia kuwa zimefanikiwa kiviwanda kwa kuhakikisha kuwa zaidi ya asilimia tisini ya viwanda walivyonavyo ni viwanda vidogo vidogo

chanzo eavt

No comments