Header Ads

Serikali imewakaribisha wawekezaji kutoka nchi ya FINLAND kuja kuwekeza katika sekta mbalimbali nchini ikiwemo ya nishati katika kipindi hiki wakati ambapo taifa la Tanzania linaelekea katika uchumi wa viwanda.

Serikali imewakaribisha wawekezaji kutoka nchi ya FINLAND kuja kuwekeza katika sekta mbalimbali nchini ikiwemo ya nishati katika kipindi hiki wakati ambapo taifa la Tanzania linaelekea katika uchumi wa viwanda.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo Ikulu jijini Dar es Salaam alipokutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Heshima wa Tanzania nchini Finland VESA VIITANIEMI.
Makamu wa Rais amesema kuwa mkakati wa sasa wa serikali ni kuhakikisha taifa linajitosheleza ipasavyo katika nishati ya umeme hatua ambayo itasaidia wawekezaji wengi kutoka mataifa mbalimbali duniani kuja kuwekeza nchini kutokana na nchi kuwa na umeme wa kutosha na wa uhakika utakaotumika katika viwanda vitakavyojengwa katika maeneo mbalimbali nchini.
Makamu wa Rais amemweleza Balozi huyo kuwa kwa sasa jitihada kubwa za Serikali ya awamu ya Tano zimeelekezwa katika uimarishaji wa miundombinu ikiwemo reli, bandari na barabara ili kurahisisha usafiri na usafirishaji wa bidhaa mbalimbali kote nchini.
Kwa upande wake, Balozi wa Heshima wa Tanzania nchini Finland VESA VIITANIEMI amemhakikishia Makamu wa Rais kuwa nchi ya Finland itaendelea kushirikiana na Serikali katika kusaidia uimarishaji wa huduma bora kwa wananchi ikiwemo kuwezesha wajasiriamali ili waweze kufanya kazi zao kwa ufanisi.
Mahusiano mazuri kati ya Tanzania na Finland yamewezesha Watanzania zaidi ya 500 kuishi nchini humo kwa ajili ya shughuli mbalimbali ikiwemo za kimasomo.
Balozi wa Heshima wa Tanzania nchini Finland VESA VIITANIEMI aliongozana na Mke wa Rais Mstaafu wa awamu ya TATU Mama ANNA MKAPA

No comments