Mkuu wa shule ya sekondari iliyopo Kishapu, mkoani Shinyanga, Marxon Paul, amevuliwa madaraka kutokana na tabia ya ulevi na kushindwa kusimamia taaluma shuleni hapo
Mkuu wa shule ya sekondari iliyopo Kishapu, mkoani Shinyanga, Marxon Paul, amevuliwa madaraka kutokana na tabia ya ulevi na kushindwa kusimamia taaluma shuleni hapo.
Hatua hiyo imechukuliwa na Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya hiyo, Stephen Magoiga, baada ya kufika shuleni hapo na kukuta mgomo uliochangiwa na tabia ya mwalimu mkuu huyo.
Kaimu mkuu wa idara ya elimu sekondari katika halmashauri hiyo, Paul Kasanda alisema mkuu huyo wa shule ameshindwa kuwasimamia walimu anaowaongoza.
“Ni kweli Mkurugenzi jana alitembelea shule hiyo na kupata malalamiko kutoka kwa wanafunzi, amechukua uamuzi wa kumvua madaraka mkuu wa shule,” alisema Kasanda.
“Tumeona tuchukue hatua stahiki dhidi ya mkuu wa shule ili iwe fundisho kwa wengine, hebu fikiria kiwango cha ufaulu kimekuwa kikishuka kila mwaka tangu 2012 katika mitihani mbalimbali wanayofanya wanafunzi,” aliongeza.
Kwa sasa shule hiyo inaongozwa na Makamu Mkuu, Marco Badalaha hadi pale uteuzi mwingine kuziba nafasi hiyo utakapofanywa na katibu tawala wa mkoa.
Post a Comment