Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mh. Paul Makonda, ameahidi kutoa shilingi milioni 2 kwa wanafunzi watatu watakaofaulu zaidi masomo ya sayansi katika mtihani wa kidato cha nne mwaka huu.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mh. Paul Makonda, ameahidi kutoa shilingi
milioni 2 kwa wanafunzi watatu watakaofaulu zaidi masomo ya sayansi
katika mtihani wa kidato cha nne mwaka huu.
Paul Makonda - Mkuu wa Mkoa wa DSM
Mbali na zawadi hiyo, mkuu huyo wa mkoa pia ameahidi kutoa ufadhili wa masomo ya kidato cha tano na cha sita kwa wanafunzi hao ambapo watapewa nafasi ya kuchagua shule yoyote wanayoitaka, na gharama zake zitagharamiwa na ofisi ya mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam.
"Mwanafunzi atakayeshika nafasi ya kwanza katika masomo ya sayansi, ya pili, na ya tatu watachagua shule yoyote waitakayo, na watasoma bure" amesema Makonda.
Makonda, ametoa pia ahadi ya shilingi milioni mbili kwa kila mwalimu ambaye atafaulisha zaidi katika masomo ya sayansi mkoani humo, pamoja na nafasi ya kutembelea mbunga yoyote ya wanyama nchini.
Post a Comment