Mgombea wa urais wa Marekani kupitia chama cha Republican, Donald Trump amekuwa akiteka vichwa vya habari kila siku – na sasa nyota yake ya heshima ya ‘Hollywood Walk of Fame’ iliyopo Los Angeles imeharibiwa.

Kipande cha video kilichochukuliwa na baadhi ya kamera zilizokuwa karibu na eneo hilo la tukio Jumatano hii zimemuonyesha mwanaume mmoja akiwa na sululu akiiharibu nyota hiyo ya heshima aliyopatiwa mgombea huyo mwaka 2007.
Matukio mengi yamekuwa yakimtokea Trump kutokana na maneno yake ikiwemo tukio lililotokea miezi michache iliyopita, mfano wa ukuta uliwekwa kuzunguka nyota hiyo iliyoharibiwa baada ya kutangaza kwamba angejenga ukuta kwenye mpaka wa Marekani na Mexico kuzuia wahamiaji wasiingie Marekani.
Tazama video ya mtu huyo akiharibu nyota hiyo.
Post a Comment