Header Ads

Leo Oktoba 29 ni siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Rais wa Tanzania Mh.John Magufuli.Tunapenda KALI ZOTE BLOG TUNAmtakia heri na baraka tele



John Pombe Joseph Magufuli (amezaliwa 29 Oktoba1959) ni mwanasiasa nchini Tanzania. Anatokea katika chama cha CCM.

Alikuwa mbunge wa jimbo la Biharamulo Mashariki katika bunge la kitaifa huko nchini Tanzania na tangu mwaka 2010 waziri wa ujenzi.

Tarehe 12 Julai 2015 alichaguliwa kuwa mgombea urais wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi na mgombea mwenza ni Samia Suluhu Hassani.

Tarehe 29 Oktoba 2015 Tume ya Taifa ya Uchaguzi ulimtangaza kuwa rais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa ushindi wa kura 8,882,935 sawa na 58.46% pamoja na makamu wa rais Samia Suluhu Hassani.

Tarehe 5 Novemba 2015 aliapishwa kama rais wa tano wa Tanzania, ingawa upinzani haujakubali matokeo hayo.
Tarehe 10 Desemba 2015 alitangaza baraza la mawaziri likiwa na watu 34 tu katika nafasi ya waziri au naibu waziri.

Ana Shahada ya Uzamivu ya Kemia (2006 – 2009) kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Pia miaka 1991 – 1994 alisomea Shahada ya Uzamili (Kemia) katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, na baadaye Chuo Kikuu cha Salford nchini Uingereza na miaka 1985 – 1988, alisoma Shahada ya Kwanza ya Elimu katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akichukua masomo ya Kemia na Hisabati. Kabla ya hapo Magufuli alisoma diploma katika Chuo cha Mkwawa akichukua masomo ya Kemia na Hisabati, hiyo ilikuwa miaka 1981– 1982.

Upande wa sekondari, Magufuli alipata elimu ya juu ya sekondari katika Shule ya Sekondari Mkwawa huko Iringa kipindi cha miaka 1979 – 1981. Kabla ya hapo miaka 1977 – 1978, alisoma elimu ya sekondari katika Shule ya Sekondari Lake, Mwanza na miaka 1975 – 1977, alisoma Shule ya Msingi KatokeBiharamulo mkoani Kagera. Hapo kati alikwenda Jeshi la Kujenga Taifa huko Arusha kwa mujibu wa sheria.
Ameandika vitabu na majarida mbalimbali..

Leo Oktoba 29 ni siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Rais wa Tanzania Mh.John Magufuli.Tunapenda KALI ZOTE BLOG TUNAmtakia heri na baraka tele










No comments