Msanii Mr. Blue ametangaza kuacha kutumia jina la Simba ambao hivi karibuni liliibua mzozo mkubwa huku mashabiki wakidai kuwa ni la Diamond Platnumz huku naye akidai jina hilo ni lake.
Msanii Mr. Blue ametangaza kuacha kutumia jina la Simba ambao hivi karibuni liliibua mzozo mkubwa huku mashabiki wakidai kuwa ni la Diamond Platnumz huku naye akidai jina hilo ni lake.
Akizungumza kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Mr. Blue amesema ameamua kucha kutumia jina hilo na sasa anatumia jina la 'Nyani Mzee', mpaka pale itakapotokea mtu mwingine na kudai pia ni lake kama ilivyojitokeza kwa Diamond Platnumz.
"Actualy Simba sasa hivi nimeiacha, sijapost siku nyingi kuhusu hilo, sasa hivi naenda kama 'Nyani Mzee' kwa sababu nyani mzee kakwepa mishale mingi sana, nasubiri na hiyo waichukue nitatafuta nyingine", alisema Mr. Blue.
Jina la 'Simba' lilileta utata mkubwa kwa baadhi ya wasanii huku wasanii wengi wakidai ni jina lao ambapo Mr. Blue alikuwa na brand ya 'Simba', na Diamond Platnumz akilitumia mpaka kwenye logo ya vitu vyake.
Post a Comment