Wanafunzi wa kidato cha nne Nchini kote wanatarajiwa kuanza mitihani yao ya mwisho,siku ya Jummane Novemba mosi mwaka huu
Wanafunzi wa kidato cha nne Nchini kote wanatarajiwa kuanza
mitihani yao ya mwisho,siku ya Jummane
Novemba mosi mwaka huu ambapo wametakiwa
kutumia muda wao kujiandaa,badala ya kuhangaika kufanya udanganyifu wa kutafuta mitihani.
Hayo yamebainishwa na makamu mkuu wa shule ya Sekondari
Buluba iliyopo katika manispaa ya Shinyanga Mwalimu MAKOYE NZALA wakati akizungumza na KALI ZOTE BLOG
COPY KWENYE MTANDAO
Amesema wanafunzi
wanapaswa kutumia muda wao kujiandaa na kuomba ushauri wa kitaaluma kutoka kwa
walimu,badala ya kuhangaika kutafuta mitihani
hali ambayo itawapotezea muda, kwani mitihani watakayopatiwa
mitaani ni bandia
--
Kwa upande wao baadhi ya wanafunzi wa shule ya Sekondari
Buluba iliyopo katika Manispaa ya Shinyanga wamesema wana uhakika wa kufanya
vizuri mitihani yao kwani wamejiandaa vyema.
----
Makamu mkuu wa shule ya Sekondari Buluba ametoa angalizo kwa
wanafunzi kutojihusisha na udanganyifu katika kipindi chote ambacho mitihani inaendelea kwani vyombo vya
usalama havitosita kuchukua hatua za kisheria dhidi ya wahusika.
Post a Comment