Header Ads

CHAMA cha Wanawake Wanasheria Tanzania TAWLA kwa kushirikiana na Asasi za kiraia na mashirika yasiyo kuwa yakiserikali yameunda mtandao wa pamoja kama hatua ya kusaidia juhudi za serikali za kupunguza au kuondoa kabisa ajali za barabarani


CHAMA cha Wanawake Wanasheria Tanzania TAWLA kwa kushirikiana na Asasi za kiraia na mashirika yasiyo kuwa yakiserikali yameunda mtandao wa pamoja kama hatua ya kusaidia juhudi za serikali za kupunguza au kuondoa kabisa ajali za barabarani

Image result for PICHA YA AJALI




Mpango huo utafanyika kwa kutoa elimu ya usalama barabarani kwa umma na kushawishi mabadiliko chanya ya sera na sheria ya usalama barabarani ziweze kuendana na wakati .
Akizungumza na Wanahabari jijini Dar es Salaam leo Mkurugenzi Mtendaji wa TAWLA Tike Mwambipile amesema kuwa kwa mujibu wa taarifa za jeshi la Polisi Nchini Tanzania asilimia 76 ya ajali za barabarani husababishwa na uzembe wa madereva na kuwa asilimia 8 husababishwa na ubovu wa barabara huku ubovu wa vyombo vya moto ukichangia asilimia 16  hali ambayo ingeweza kuepukika endapo watumiaji wa barabara wangezitii sheria na kanuni za usalama barabarani.
Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Sheria kutoka Makao Makuu ya Jeshi ya Polisi ASP Deus Sokoni amebainisha kuwa sheria ya usalama barabarani ya mwaka 1973 imeelezea visababishi vikuu vine vya ajali za barabarani kwa ufasaha ambavyo ni Matumizi mikanda, matumizi sahihi ya kofia ngumu, matumizi ya vilevina uendeshaji wa vyombo vya usafiri pamoja na mwendokasi isipokuwa vizuizi vya watoto ambayo haijaelezewa kabisa katika sheria hiyo.
Naye Mkurugenzi wa taasisi binafsi ya Safe Speed Foundation Henry Bantu amebainisha kuwa ajali za barabarani zinaweza kuepukika endapo kutakuwa na juhudi za pamoja za dhati pamoja za wadau wa usalama barabarani na utashi wa kisiasa  wa wanasiasa ambao ndiyo watunga sera na sheria   hizo

No comments