Header Ads

Dance100% imebadilisha imewaka bidhi washindi kombe


 

Dance100%  imewaka bidhi washindi kombe 

 

 

Washindi wa shindano la kusaka vipaji la Dance100% 2016 Team Makorokocho wamesema baada ya ushindi huo wameimarika zaidi na kujenga umoja ambao utawawezesha kufikia malengo yao katika sanaa . 





Team Makorokocho

Wakizungumza katika kipindi cha 5SELEKT kinachorushwa na EATV wamesema baada ya ushindi huo wameweza kupanga nyumba pamoja kutokana na kupata ugumu kila walipotaka kukutana kwa ajili ya mazoezi.

“Imebidi tupange nyumba ya pamoja Temeke Jijini Dar es Salaam kwa kuwa tulikuwa tunakaa mbalimbali sana na kwa foleni ya Jiji tukawa tunashindwa kufanya kazi kwa wakati, kwa sasa tumekuwa na ushirikiano wa kutosha na tunazidi kufanya vizuri katika sanaa zetu” Amesema  Hamad Abasi mmoja wa wanakundi hilo.


 
Aidha baada ya kujinyakulia kitita cha milioni 7 za shindano la Dance100% waliweza kuzitumia kwa kuwapa wazazi wao fedha kidogo na nyingine wakagawana na kubakiza kidogo kwa ajili ya mfuko wa kundi lao.

Pamoja na hayo kundi hilo limesema linajifua zaidi katika sanaa ya uchezaji ili kushiriki mashindano yatakayojitokeza pamoja na shughuli mbalimbali za kijamii.

No comments