Header Ads

Msimu mpya wa Ligi ya Mpira wa Kikapu nchini Marekani NBA, unatarajiwa kuanza kesho,

Msimu mpya wa Ligi ya Mpira wa Kikapu nchini Marekani NBA, unatarajiwa kuanza kesho,          ambapo mabingwa watetezi wa michuano hiyo Cleveland Cavaliers, wanaanza kampeni yao,               kwa kuwaalika New York Knicks, mchezo utakaopigwa Quicken Loans Arena.  


Nao washindi wa pili wa michuano hiyo, msimu uliopita, Golden State Warriors wataikaribisha, San Antonio Spurs, pale Oracle Arena, wakati Portland yenyewe pia itakuwa mwenyeji wa Utah               Jazz.
Mchezaji Dwayne Wade, anatarajiwa kuchezea kwa mara ya kwanza timu yake mpya ya Chicago Bulls, baada ya kuachana na Miami Heats aliyoitumikia kwa misimu 13.




No comments