Habari kuu leo Jumatano
Habari kuu leo Jumatano
Mkurugenzi mkuu wa
idara ya upelelezi nchini Marekani, James Clapper, amesema kuwa sera ya
kujaribu kuishawishi Korea Kaskazini, kuachana na mpango wake wa kuunda
zana za kinuklia, bila shaka ni kupoteza muda bure. Katika hotuba,
amesema kuwa la muhimu kwa Marekani kufanya ni kuidhibiti taifa hilo ili
lisiendelee na azma yake ya kuunda zana hizo za kitonoradi.
Bunge
la Congress nchini Venezuela, limepiga kura ya kuanzisha kesi ya
kisiasa dhidi ya Rais wa chama cha Kisosiolisti, Nicolas Maduro, na
kusababisha taharuki zaidi kati ya serikali na bunge la kitaifa,
linaloongozwa na wanasiasa wa upinzani. Bunge hilo la Congress,
linamtuhumu Bwana Maduro, kwa ukiukaji wa demokrasia.Serikali ya Gambia, inasema kwamba itajiondoa mara moja, kutoka mahakama ya kimataifa ya makosa ya jinai-ICC, huku ikiilaumu kwa kuwahukumu waafrika pekee. Uamuzi huo unafuatia ule wa Afrika Kusini na Burundi, ya kujiondoa kutoka katika mahakama hiyo, iliyoko The Hague nchini Uholanzi. Rais Yahya Jammeh, ametawala Gambia tangu alipochukua uongozi kwa njia ya mapinduzi, mwaka 1994. Muendesha mashtaka mkuu wa sasa wa ICC, Fatou Bensouda ni mzaliwa wa Gambia.
Mgombea kiti cha Urais wa chama cha Republican Nchini Marekani Donald Trump, amesema kuwa sera za kigeni za mpinzani wake Bi Hillary Clinton kuhusiana na Syria, itasababisha vita kuu ya tatu ya Dunia. Bwana Trump, amesema Marekani inafaa kulenga kuliangamiza kundi la Islamic State, badala ya kujaribu kumshawishi Rais wa Syria, Bashar al-Assad, kujiuzulu.
Post a Comment