Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya sekondari ya Buluba iliyopo mjini Shinyanga wamesema mimba mashuleni husababisha madhara mbalimbali ikiwa ni Pamoja na kuwepo kwa ongezeko la watoto wa mitaani.
Baadhi ya wanafunzi wa
Shule ya sekondari ya Buluba iliyopo mjini Shinyanga wamesema mimba mashuleni
husababisha madhara mbalimbali
ikiwa ni Pamoja na kuwepo kwa ongezeko
la watoto wa mitaani.
Add caption |
Wakizungumza na KALI ZOTE BLOG leo,wamesema mimba mashuleni husababisha kukatisha
malengo,ongezeko la watoto mitaani na madhara mengine mengi
---
Wametaja sababu
zinazopelekea wanafunzi kupata ujauzito kuwa ni kukosa hofu ya
mungu,vishawishi,lakini pia wazazi kukumbatia mila kandamizi inachangia, Pamoja
na sababu nyinginezo.
Mmoja wa wanafunzi hao
Yohana Bartazar Kija ameomba mamlaka zinazohusika na maamuzi kuhakikisha
zinazimamia sheria ikiwa ni Pamoja na kudhibiti mianya ya rushwa ili kuwabana watuhumiwa wanaohusika na
matukio hayo
.
Kwa upande wake makamu
mkuu wa shule ya sekondari Buluba mwalimu MAKOYE NZALA amesema Pamoja na vyanzo
vingine lakini utandawazi ni moja ya sababu zinazowasababishia wanafunzi kupata
ujauzito.
…..
Mwalimu NZALA ameomba
elimu ya Jinsia iendelee kutolewa hasa mashuleni kuhusu madhara ya kujihusisha
na mapenzi katika umri mdogo
Post a Comment