Mauaji ya vikongwe,umasikini,ushirikishwaji hafifu katika Nyanja mbalimbali ni baadhi ya changamoto zinazowakabili wazee
Mauaji ya
vikongwe,umasikini,ushirikishwaji hafifu katika Nyanja mbalimbali ni baadhi ya
changamoto zinazowakabili wazee
Akizungumza katika
mkutano uliohusisha waandishi wa habari na viongozi baraza la
wazee wa wilaya ya Shinyanga,Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga JOSEPHINE MATIRO ametaja changamoto
mbalimbali zinazowakabili kundi hilo ikiwemo mauaji
Mheshimiwa
MATIRO amesema mauaji hasa kwa wanawake yameendelea kuwanyima amani
wazee na kuwaweka katika hali ya wasiwasi.
Mmoja wa viongozi
katika baraza la wazee BONIFAS BOAZ
ameeleza adha wanazokumbana nazo wazee wakati wa upatikanaji wa huduma katika
baadhi ya vituo vya afya.
Amesema serikali ipo
tayari kuweka mazingira rafiki kwa wazee ikiwa ni Pamoja na kuweka mikakati ya
kukabiliana na changamoto hizo sambamba
na kuwakamata watuhumiwa wanaojihusisha na mauaji ya vikongwe.
Amesema wazee ni hazina
na kwamba serikali inatambua mchango wao
katika ujenzi wa taifa la Tanzania
Post a Comment