Hadi samaki 80,000 aina ya rainbow trout wanaofugwa wameachiwa kimakosa baharini Denmark,
Hadi samaki 80,000
aina ya rainbow trout wanaofugwa wameachiwa kimakosa baharini Denmark,
na wito sasa umetolewa kwa wavuvi kujaribu kuwakamata.
Kuna hofu kuwa samaki hao walio na uzito wa kilo 3, huedna wakatiza vizazi vya aina nyengine ya samaki.
Mwanamazingira mmoja ameomba "yoyote aliye na vifaa vya uvuvi... akavue".
Soren Knabe, mwenyekiti wa kundi la kimazingira Vandpleje Fyn na mwenyekiti wa muungano wa wavuvi Denmark, ameliambia gazeti la Copenhagen post kuwa huu ni muda mbaya zaidi kwa samaki hao kuingia katika bahari hiyo.
'Bahati mbaya'
Meli hiyo ya mizigo ilikuwa inatoka Kalinigard Urusi kuelekea katika bandari ya Kolding Denmark ilipoingia katika sahmba hilo la ufugaji samaki.
Jon Svendsen, mtafiti wa taasisi ya National Institute of Aquatic Resources, amesema samaki hao ni tisho kwa kizazi cha samaki wa baharini kwasababu wanaweza kuchimba kutafuta mayai ya samaki na kuyala.
Amesema hiyo inaweza kuathiri moja kwa moja mazingira nani 'bahati mbaya' ajali hii imetokea sasa.
Dr Svendsen ameshinikiza wito kuwa wavuvi wajaribu kuwavua samaki hao. Hatahivyo amesema tihiso hilo sio la muda mrefu.
Tishio kubwa zaidi kwa mazingira amesema ni kuchotwa mchanga wa baharini kwa ujenzi , shughuli za viumbe visivyo vya baharini, mabadiliko ya hali ya hewa na mashamba yenyewe ya kufuga samaki.
CHANZO BBC
Post a Comment