Msanii na mtayarishaji wa muziki wa High Table Sound, Barnaba Classics amesema pesa zikimtembelea atajenga kanisa.
Msanii na mtayarishaji wa muziki wa High Table Sound, Barnaba Classics amesema pesa zikimtembelea atajenga kanisa.
Muimbaji huyo ambaye pia huwaandikia wasanii nyimbo za gospel, alisema hawezi kuwa muhubiri bali atafanya issue tofauti ambazo zitampendeza mwenyezi mungu.
“Mimi siwezi kuja kuwa muhubiri ila nikija kupata hela kupitia muziki nimepanga kuja kutengeneza kanisa ili liweze kutoa huduma kwa wanaumini ila si kuhubiri kanisani kama ambavyo shabiki wangu alivyosikia huko mitaani,” Barnaba alikiambia kipindi cha Planet Bongo cha EA Radio.
Mbali na hilo msanii huyo alisema kuwa kwa sasa yeye hana muda wa kumfundisha mtu jinsi ya kuimba bali anaweza kumpiga msasa mtu ambaye tayari anaweza kuimba kwani yeye muda wa kumfundisha mtu kwa sasa hana.
“Mimi saizi kiukweli sifundishi mtu namna ya kuimba kwani sina muda wa kufundisha mtu ila kama mtu unakipaji naweza kukupiga msasa ukafanya vizuri ila si kufundisha mtu” alisema Barnaba
Post a Comment