Header Ads

Msanii Nikki wa Pili anayeunda kundi la Weusi, ambaye pia ni msomi wa chuo kikuu, amezungumzia tuzo za EATV na kusema kuwa ni watu sahihi kuanzisha tuzo kwani ni watu wanaoijua sanaa.



Msanii Nikki wa Pili anayeunda kundi la Weusi, ambaye pia ni msomi wa chuo kikuu, amezungumzia tuzo za EATV na kusema kuwa ni watu sahihi kuanzisha tuzo kwani ni watu wanaoijua sanaa.

 




Akizungumza na EATV Nikki wa Pili amesema EATV kuanzisha tuzo ni sawa na mwanafunzi kukutana na mwalimu sahihi wa somo husika, kwani ana imani itainua sanaa ya Tanzania.

“Media ni mdau moja kwa moja wa muziki, mziki unapigwa hapo, movie zinaruka hapo, kwa hiyo nje ya kwamba hawa ni wadau lakini pia ni watu wenye ufahamu mkubwa sana, kwa hiyo nafikiri media kutoa tuzo ni kama mwanafunzi amekutana na mwalimu hasa wa lile somo, ni kitu kizuri ni platform yenye nguvu sana”, alisema Nikki wa Pili.

Nikki wa pili aliendelea kusema kuwa EATV AWARDS zitaongeza wasifu mkubwa kwa wasanii na thamani yao, pamoja na kuwafanya kutambulika duniani kwa kazi zao nzuri.

“Definetely inaongeza thamani ya muziki, inaongeza ushindani na inatoa nafasi ya wengi kufuatilia muziki, lakini pia inajenga CV, unapopata tuzo inakujengea CV popote utapoenda ulimwenguni watu wanakutambua kwamba ulikuwa awarded”, alisema Nikki wa Pili.

No comments