Mwakilishi mkazi wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF nchini Tanzania Maniza Zaman na mwakilishi mkazi wa Burundi Bo Victor wamefanya ziara ya pamoja kwenye kambi za wakimbizi wa Burundi nchini Tanzania
Mwakilishi mkazi wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF nchini Tanzania Maniza Zaman na mwakilishi mkazi wa Burundi Bo Victor wamefanya ziara ya pamoja kwenye kambi za wakimbizi wa Burundi nchini Tanzania.
Wawakilishi hao wamezuru kambi za Nyarugusu, Nduta na Mtembeli zilizoko mkoani Kigoma nchini Tanzania ambapo zaidi ya nusu ya watoto wote kwenye kambi hizo ni wakimbizi kutoka Burundi.
Maniza Zaman amesema lengo la ziara yao lilikuwa ni kungalia hali katika kambi hizo za wakimbizi lakini pia kuangalia upande wa serikali hapo kipaumbele chao na jinsi gani ya kuweza kuzisaidia jamii zinazowahifadhi ambapo amesema kilichomuhuzunisha zaidi ni kwamba asilimia karibu 60 ya wakimbizi hawo ni watoto
Kwa upande wake mwakilishi wa Burundi Bwana Bo amesema hali waliyoshuhudia katika siku tatu za ziara yao inaridhisha licha ya changamoto zilizopo na kwamba kubwa kwake ni suala la elimu kwa sababu mitaala ya elimu ya Tanzania ni tofauti na nchini Burundi
CHANZO EATV
Post a Comment